Promote your business for free

THIS BLOG IS SPONSORED BY AFRICAN SOCIAL NETWORK ,THE SOCIALY NETWORK PAY ITS USER IN POINTS BASED JOIN NOW AND SEE HOW MUCH MONEY YOU CAN MAKE USING SOCIAL NETWORK. | FEEL FREE TO ADVERTISE ON WWW.BONGLOB.COM

Tuesday, 31 August 2010

NAFASI YA MAFUNZO

Tunafuraha kukujulisha kuwa TA Reading & Berkshire wakishirikiana na ACCG ya hapa Reading wanakuletea mafunzo ya jinsi ya kuandika CV na kujieleza kwenye Interview (usaili). Yatakayo fanyika katika ukumbi wa RISC London Street tarehe 09/09/2010.

Kutokana na Watanzania kuwa tumesoma na kuwa na vyeti ambavyo tunaweza kupata kazi nzuri, lakini kutokana na matatizo mbali mbali tumekuwa hatuwezi kupata kazi hizo katika maeneo tuliyosomea.

Kwa mfano mtu ana Master degree ya Accounts lakini anafanya kazi ya care na wala siyo ya kuajiriwa bali anakwenda kwa kutumia wakala. Sasa tunataka kuwasaidia wale wote wenye nia ya kufanya kazi kutokana na kile ambacho wamesomea.

Mafunzo hayo yatafanywa na wataalamu ambao wanawasaidia watu kurudi makazini na kuna uwezekano wa kuweza kuwapatia kazi pia.

Hata kwa wale wanafunzi ambao bado hawajamaliza nao pia wanasaidiwa kupata replacement kwenye eneo ambalo unasomea.

Kutakuwa na kuchangia kidogo kwa wale watakao taka hayo mafunzo na ni pound tano (£5) kwa kila mtu, Na unatakiwa kujiandikisha kwani nafasi ni chache.

Unaweza kutuma barua pepe ya kushika nafasi lakini utatakiwa ulipe kabla ya tarehe 07/09/2010.

Wasilisha malipo yako ofisini 35-39 London Street.

Wote mnakaribishwa na mjulishe na mwenzio.

No comments:

Post a Comment