Watu waliohusika katika mafunzo hayo ya kuandaa cv nzuri na jinsi ya kujibu maswali wakati wa interview wamekua wazi kabisa na kuona wenyewe ni jinsi gani watu hukosa kazi sio kwa ajili hawajasoma ila ni kwasababu ya kuwa na cv yenye muonekano mbaya na jinsi ambavyo wanajibu maswali wakati wa interview.
imekua ni siku maalumu sana kwani watu wameondoka wakiwa wameelimika kabisa na kuombwa waone jinsi ambavyo wanaweza kufanya kazi bila malipo (volunteer) ili Kupata fursa ya kutengeneza cv zao. Picha hapo chini ni za leo kwenye training .
ND;James Ahadi akiwa na Abduli Shelufumo wakiwa wanafanya kazi ya kurekebisha cv mbovu za watu zilizo tumwa kwenye makampuni mbalimbali na kuzitoa makosa ili kuwawezesha wengine kuona jinsi ya kuandika cv.
Ilikua ni fursa ya kipekee kuhudhuria mafunzo hayaa, nakujihisi tofauti kubwa tu mara baada ya kumaliza hili zoezi, tunawashukuru viongozi wetu kwa kuwa nasi bega kwa bega kuhakikisha watanzania tunapata kinachostahili kwa maslahi yetu na taifa.
ReplyDelete