Tanzania na nchi nyingine mbalimbali za kiafrika zinaweza kunufaika zaidi kama zitaweka kipaumbele utumiaji wa nishati endelevu
(Sustainable Energy) hususani vijiji ili kuleta maendeleo na kupunguza umasikini. Nishati endelevu hutoka kwenye mwangaza wa Jua, Maji, Takataka na Kinyesi cha binadamu na wanyama. Hizi nishati mbadala hutoa umeme na gesi ambazo hutumika majumbani kwa kupikia na kuwasha taa hivyo kusaidia kutunza mazingira yetu na kuondoa utumiaji wa mkaa unaosababisha uharibifu wa mazingira kwa ukataji ovyo wa miti
Urban Pulse inawaletea documentary sehemu ya Pili kwenye version ya kiswahili, Documentary hii mpya ambayo tayari imerushwa hewani kwenye vituo tofauti vya Televiseni za nchi mbalimbali za bara la Ulaya na Afrika na imetafsiriwa katika lugha saba mbalimbali.
Documentary hii ambayo Ashden wali wa kamishen URBAN PULSE kuizalisha inaonyesha na kuhamasisha wajasilimali, wananchi namna gani nchini za kiafrika zinavyonufaika na misaada hii kutoka shirika la hili la Ashden Awards For Sustainable Energy.
Shirika hili ambalo lina saidia kukuza utumiaji wa nishati endelevu, lina saidia uboreshaji na utunzaji wa mazingira duniani . Shirika hili liliundwa na duka maarufu la familia ya kitajiri ya Sainsbury. Mlezi wa shirika hili ni Mwana Mfalme wa Wales Charles Philip Arthur George
Hi ni mojawapo ya project kubwa ambazo zinazalishwa kwenye studio za Urban Pulse Creative
No comments:
Post a Comment