Promote your business for free

THIS BLOG IS SPONSORED BY AFRICAN SOCIAL NETWORK ,THE SOCIALY NETWORK PAY ITS USER IN POINTS BASED JOIN NOW AND SEE HOW MUCH MONEY YOU CAN MAKE USING SOCIAL NETWORK. | FEEL FREE TO ADVERTISE ON WWW.BONGLOB.COM

Sunday, 12 September 2010

SHUKRANI KWA WANAJUMUIYA WOTE

Viongozi pamoja na Jumuiya ya watanzania Reading, ingependa kutoa Shukurani za dhati kwa wale wote waliotusaidia katika kufanikisha Pambano la mechi ya Mpira wa Miguu liliofanyika kwa mafanikio makubwa hapa Reading tarehe 11/09/10, ktk viwanja vya Kensington.

Kwanza kabisa tungependa kuwashukuru wachezaji wote wa TZ Reading Mlioshiriki, pamoja na uongozi wenu kwa kukubali kuwa na mechi hii bila ubishi wowote au maswali maswali. Tumefanya kazi pamoja na kuandaa mechi kwa kipindi kifupi kabisa, asanteni sana kwa utayari wenu, tunaamini huu ushirikiano hautaishia hapo.

Tungependa kutoa shukurani za dhati kwa wafuatao ambao wametoa fedha zao ili kusaidia tukio hili liweze kufanikiwa:

Familia ya bwana na bibi Mbarukh MZEE, kwa kuchangia fedha.
Bongo Flava kwa kuchangia fedha.
Na COSTCO (kupitia Katibu wa TA READING) kwa kutupatia mipira ya zawadi za wachezaji.

Hawa ndio watu wachache waliotoa fedha zao kuchangia tukio hilo la Mpira wa miguu kati ya TZ Reading FC na TZ Milton Keynes FC.

Tunawashukuruni sana kwa moyo huo mlioonyesha na Mungu awabariki sana.

Pia kwa wale wote waliojitahidi kufika uwanjani kusupport timu zetu, tunawashukuru sana kwa muda wenu.

Tunamshukuru Mwenyekiti wa TA Taifa kwa muda aliojitolea kukaa uwanjani pamoja na kuwa na majukumu mengine mengi kwa siku hiyo, lakini alivumilia mpaka mwisho wa mechi na kutoa zawadi kwa washindi; asante sana Mwenyekiti.

Tukio hili limekuwa la mafanikio makubwa na tumeona ni jinsi gani kwamba nia yetu ya kuendeleza na kudumisha Umoja kati ya watanzania hapa Uingereza, huku tukiinua vipaji vya mpira wa miguu kwa watanzania, linaweza kufanikiwa kabisa.

kwa wale ambao hawakuwepo mpirani ningewashauri msikose tena mechi nyingine ikiandaliwa, kwani tukio hili lilifana sana na Mungu akituwezesha tutaandaa lingine, karibuni.

Asanteni wote

UONGOZI TA READING

No comments:

Post a Comment