Promote your business for free

THIS BLOG IS SPONSORED BY AFRICAN SOCIAL NETWORK ,THE SOCIALY NETWORK PAY ITS USER IN POINTS BASED JOIN NOW AND SEE HOW MUCH MONEY YOU CAN MAKE USING SOCIAL NETWORK. | FEEL FREE TO ADVERTISE ON WWW.BONGLOB.COM

Tuesday, 14 September 2010

Tanzania yawa na leseni za maana sasa





J.R. Whipple & Associates

Tunasomeka duniani kwamba tupo sasa baada ya kupata leseni mpya. Hongera kwa nchi yetu jamani.





Mkurugenzi wa huduma kwa mlipa kodi, Mamlaka ya Mapato (TRA), Protas Mmanda, akionyesha mfano wa leseni mpya za udereva, makao makuu ya TRA jijini Dar. Shoto ni Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Polisi wa usalama barabarani, Johansen Kahatano. Habari na http://www.wavuti.com/
Picha na Chachandu Daily blog.

Mamlaka ya mapato Tanzania, TRA, kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini wameanza utekelezaji wa mfumo mpya wa utoaji leseni za udereva wa vyombo vya moto kwa lengo la kudhibiti ajali za barabarani na utoaji holela wa leseni na kudhibiti mapato ya Serikali.


Kadhalika, Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Polisi wa Usalama Barabarani, Johansen Katahano, amesema kuwa madaraja ya leseni hizo yameongezwa kutoka 8 hadi 14. Madaraja hayo yameongezwa katika daraja A na C na yameongezwa kutokanana na uwezo wa vyombo vya moto vya madaraja husika na idadi ya abiria watakaobebwa na vyombo hivyo.


Uzinduzi wa matumizi wa leseni hiyo yatafanyika
kesho Jumatano jijini Dar.


Leseni hizo mpya zitakuwa na uwezo wa kutunza kumbukumbu za kielektroniki za mtumiaji ikiwemo idadi ya makosa aliyoyafanya akiendesha chombo cha moto, gari na pikipiki.


Leseni hizi mpya zitahitimisha matumizi ya leseni za zamani.


Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi wa TRA, Protas Mmanda amewataka madereva wanaotumia leseni zao za kawaida kutokuwa na wasiwasi kwani kwa muda huu wataendelea kutumia leseni hizo kihalali na watapewa leseni mpya watakapokuwa wanakwenda kwa ajili ya kuzihaishi. Watu wenye leseni za Daraja C wataanza kupata leseni hizo mara moja lakini watahitajika kupata mafunzo maalumu kwanza.



 

No comments:

Post a Comment