Promote your business for free

THIS BLOG IS SPONSORED BY AFRICAN SOCIAL NETWORK ,THE SOCIALY NETWORK PAY ITS USER IN POINTS BASED JOIN NOW AND SEE HOW MUCH MONEY YOU CAN MAKE USING SOCIAL NETWORK. | FEEL FREE TO ADVERTISE ON WWW.BONGLOB.COM

Tuesday 5 April 2011

Sherehe za kumkaribisha Balozi




Jumuiya ya Watanzania – Tanz UK kwa kushirikiana na T.A Reading inapenda kuchukua nafasi hii kuwakaribisha rasmi Watanzania wote katika sherehe za kumwalika balozi wetu mpya MH. Peter Kallaghe pamoja na mke wake.
Ratiba ni kama ifuatavyo:
Ijumaa, Tarehe 8/04: Saa 12 (6:00 pm) jioni: Balozi atakaribishwa na viongozi wa Jumuiya.
Jumamosi, Tarehe 9/04: Saa 5 (11:00 am) asubuhi – Saa 9 (3:00pm) Mchana: Balozi atatembelea jumuia na miradi mbalimbali ya kitanzania hapa Reading. Pia Mama balozi atakutana na wakina mama.
Kuanzia Saa 12 Jioni: Balozi atakutana na Watanzania wote katika sherehe za kumkaribisha iliyoandaliwa na Jumuiya kwa kushirikiana na Bongo Djs katika ukumbi wa Wycliffe 233 Kings Road, Reading, Rg1 4ls.
Jumapili,Tarehe 10/04: Balozi kujumuika katika ibada ya kiswahili ambayo itahitimisha ziara yake.
Kwa Maelezo zaidi wasiliana na Ndg. Hussein 07865673756, Ndg. Upete 07796122127, Mama Maria 07919874182.
Mjulishe na mwenzio.
Asanteni.

No comments:

Post a Comment