Promote your business for free

THIS BLOG IS SPONSORED BY AFRICAN SOCIAL NETWORK ,THE SOCIALY NETWORK PAY ITS USER IN POINTS BASED JOIN NOW AND SEE HOW MUCH MONEY YOU CAN MAKE USING SOCIAL NETWORK. | FEEL FREE TO ADVERTISE ON WWW.BONGLOB.COM

Sunday, 25 April 2010

Uzinduzi wa libeneke la afroIT huko china
Ukurasa mkuu wa AfroIT Mdau akimwaga sera katika hotuba ya uzinduzi wa AfroIT
Mdau akichangia mada katika uzinduzi wa AfroIT
AfroIT crew na baadhi ya wageni waalikwa
Wadau wakifuatilia uzinduzi wa AfroIT
Ankal Michuzi!
Pole na majukumu ya kuendeleza libeneke la globu yetu ya jamii. Naomba uwatambulishe wanajamii libeneke la
www.afroit.com ambapo mnamo Ijumaa tar 23 Apr
kulifanyika uzinduzi rasmi wa tovuti yetu
katika jiji la Wuhan hapa China. 1.Utangulizi AfroIT Group ni kikundi cha Watanzania wachache ambao ni vijana waliojikita kwenye uwanja wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) wakiwa na azma ya kuwafahamisha, kuwaelimisha na hata kuwajulisha Watanzania masuala mbalimbali yahusuyo ICT kupitia njia ya mtandao(yaani kupitia tovuti yetu ya www.afroit.com). 2.Azma Kama nilivyodokeza hapo awali, azma yetu hasa ni kutoa ufahamu na elimu kwa ndugu zetu watanzania katika uwanja wa teknolojia ya habari na mawasiliano. Kwa mantiki hii, tunaamini AfroIT inaweza kuwa msaada kwa jamii nzima kuanzia wanafunzi hadi wananchi wa kawaida mwenye kiu na uhitaji wa nyenzo muhimu ktk ICT. 3.Kilichomo AfroIT Ndani ya tovuti yetu, kuna kurasa mbalimbali ambazo tumezigawanya ktk makundi matano ambayo ni "e-learning", "technology", "forums", "blog" na "downloads".Hivyo basi kupitia kurasa hizi : utaweza soma vijarida na vitabu mbalimbali kuangalia video mbalimbali za masomo kuuliza yale yanayokutatiza na kuchangia mada mbalimbali kupakua(kudownload) vitabu mbalimbali kwa urahisi kukutana na habari mbalimbali zinazojiri katka ulimwengu wa ICT Hivyo basi ni tumaini letu kuwa ndugu zetu Watanzania mtauthamini mchango wetu na tunategemea kuungwa nanyi mkono katika ushauri, mawazo na hata kukosolewa inapobidi. Kwa ushauri, maswali au maoni wasiliana nasi kupitia anwani zifuatazo: info@afroit.com
au
webmaster@afroit.com Tembelea www.afroit.com leo kwani "elimu ni ushindi"

No comments:

Post a Comment