Uongozi wa Ta Reading ungependa Kukutana na watu wote ambao wamesomea mambo ya IT waishio Reading na eneo lote la Berkshire. Lengo kuu ni kuweza kuona jinsi ya kusaidiana katika mambo mbali mbali katika taaluma hii. Moja ya mambo tutakayo kuwa tunazungumzia ni namna gani ya watu kupata kazi katika makampuni makubwa ya IT, Pia kupeana taarifa za nafasi za kazi, vyuo na ofa mbali mbali zilizoko katika taaluma hii.
Tungependa pia kupata mawazo yenu jinsi jumuiya yetu itakavyoweza kwa kushirikiana na wataalamu katika nyanja hii kuweza kuwafikia wana jamii kirahisi na pia kutoa elimu kwa jamii.
Ulimwengu wa sasa wa sayansi ni muhimu tusiwe nyuma katika kushirikiana katika kujiendeleza na kwenda na wakati.
Kwahiyo ni muhimu kwa kila mwanajamii kujitokeza katika kikao hichi ambacho kitakuwa cha kwanza cha aina hii. Sio lazima uwe umesomea mambo ya IT, kwani hata kuja na kusikia nini kinachozungumziwa unaweza kutoa mchango wako. Pia tunahitaji watu waliosomea mambo yote yanayohusu computer kwa ujumla.
Sehemu itakayofanyika kikao hicho ni
Vincent Restaurant
Oxford Road
Reading.
SAA 5 asubuhi (11am) Mpaka 7 mchana (1pm)
Tarehe 22 may 2010
Kwa Masiliano Zaidi/:-
Simu 07865673756/
E-mail tzra2009@gmail.com
TA TEAM
/
/
No comments:
Post a Comment