Uongozi wa muda wa jumuiya ya watanzania London umekamilisha kazi mliyotupa ya kutengeneza mfumo mpya wa kiuendeshaji pamoja na kuitisha uchaguzi wa viongozi. Sasa tuko tayari kuwakilisha taarifa hii kwenu wanajumuiya. Shughuli hii itafanyika Ijumaa tar 14-May 10 kuanzia saa 11 jioni. Uchaguzi wa viongozi wa kudum utafanyika tar 5-June 10 na ili kufanikisha hayo kikao hiki ni muhimu sana hivyo tunaomba ushirikiano wenu, mhudhurie na kutupa mawazo pale inapohitajika.
Agenda:
--MFUMO: mfumo mpya wa kiutendaji
--KATIBA: kuichambua katiba yetu
--UCHAGUZI: kupata wagombea na upigaji kura.
--KUSIMIKWA: maandalizi ya kusimika viongozi wapya
--BALOZI: kuhusu wanajumuiya kumuaga balozi na kuwasimika viongozi
--ADA: ada za uanachama, kiasi cha kulipa na jinsi ya kulipa
--Mengineyo
Fika mapema, sote tutakuwa pale tayari kayapitia hayo yote.
-Kikao: kikao cha wanajumuiya
-Waalikwa: watanzania London
-Mahali: TANZANIA HIGH COMMISSION, 3 Stratford Place W1C 1AS, London.
Muda: Saa 11 jioni
N.B: Iweke tarehe 5 June kwenye ratiba yako, inaandaliwa party safi.
G Mboya - TA Director of Communication
No comments:
Post a Comment