Promote your business for free

THIS BLOG IS SPONSORED BY AFRICAN SOCIAL NETWORK ,THE SOCIALY NETWORK PAY ITS USER IN POINTS BASED JOIN NOW AND SEE HOW MUCH MONEY YOU CAN MAKE USING SOCIAL NETWORK. | FEEL FREE TO ADVERTISE ON WWW.BONGLOB.COM

Friday, 11 June 2010

MKUTANO NOVOTEL HOTEL READING

WAZIRI KUKUTANA NA WATANZANIA UK


Waziri wa Afrika Mashariki Dr. Deodoras Kamara anategemewa kufanya ziara ya siku tatu kuzungumza na wanajumuiya wa hapa Uingereza. Ziara hii ni kwa ajili ya kuchambua na kupata mawazo mbalimbali kutoka kwa watanzania waishio Uingereza kuhusu maswala ya Afrika Mashariki (uhamiaji, soko huria, umuliki wa ardhi, biashara, n.k). Ziara hii inafuatia ahadi aliyoitoa Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda alipoitembelea jumuiya hivi karibuni.

Tungependa watu watume maswali yao kwetu kwa kutumia barua pepe ya jumuiya ya Reading. Itasaidia kupunguza muda wa kila mtu kuuliza maswali. Maswali utakayo tuma atasomewa Mh Dr Kamara kwenye mkutano kwahiyo itasaidia vile vile hata kama utashindwa kufika utakuwa na wewe umechangia kwa kuuliza au kutoa maoni yako. Tutajitahidi kuchukua majibu ya maswali yote yatakayojibiwa na tutajitahidi kuja kuyaweka majibu ya maswali ambayo yameulizwa kwenye blog kwa kila mtu kusoma.



Kabla ya kuanza kwa mkutano na Mh waziri, wakina Mama wa Reading watakutana na kiongozi wa kinamama wa taifa ambaye ni Makamu wa Mwenyekiti Taifa. Bi Nsemwa. Ambao utakuwa katika ukumbi huo kuanzia saa saba mchana mpaka saa nane. (1pm – 2pm). Wakina Mama wote mnakaribishwa kwenye kikao hicho kitakacho kuwa kikijadili maswala ya maendeleo ya jamii kina mama na watoto. Kwa maelezo zaidi wasiliana na Bi Wendy Namba 07897277303.

Kwa hapa Reading itafanyika tarehe 19 June 2010 Kuanzia saa Nane Mchana (2pm) mpaka saa Kumi na moja jioni (5pm) Siku ya jumamosi.



UKUMBI NI:- NOVOTEL HOTEL

25B FRIAR STREET

READING

RG1 1DP

Mjulishe na mwenzio kuhusu mkutano huu, kufika kwako ni mafanikio ya mkutano huu.



Ukituma barua pepe usipopata majibu baada ya masaa kumi na mbili tangu utume tunaomba ufwatilie kwa simu ili kuhakikisha kuwa tumepata. Kwani tunapenda kila mmoja atakayetuma swali au maoni yake yaweze kujumuishwa katika taarifa yetu ya jumuiya.



Vile vile tutakuwa na taarifa fupi ya vitu tulivyofanya, mipango na maendeleo ya jumuiya yetu hapa reading.

Tunaomba ushirikiano wenu katika kuipeleka jumuiya yetu hapa Reading mbele, mchango wako wa mawazo na matendo niwa muhimu sana.

2 comments:

  1. kwa kweli sikutegemea kuona idadi ya watu wachache namna hii,inaonyesha uongozi mpya wa TA Reading umeshindwa kazi kabisa.Mwenyekiti na timu yenu nzima tokeni hamfai kabisa ,ni heri uongozi uliopita ulikuwa na nguvu sana.

    Mdau Reading

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli wana London nawashukru sana kwa jumuiya yenu,inaonekana kulikuwa na watu wengi.Ila Reading kulikuwa hakuna kitu inaonekana walikuwa hawakujiandaa kabisa ,inakuwaje sehemu maarufu kama hii inayosifika kupata watanzania 15-20 .Jana ilikuwa aibu tupu hata kinywaji kwa wageni kulikuwa hakuna kabisa.wageni waalikwa walishindia maji ya kunywa na karanga kumi kwenye mfuko.Mwenyekiti wa Jumuiya ya Reading hawezi kabisa bora ajiuzulu kabisa.Nini kimeikumbuka Jumuiya nzito kama hii?Baadhi viongozi wa juu wa ccm kuanzia tawi hadi shina.Tunaomba mwenyekiti na safu yako Mjiuzulu kazi imewashinda ,jumuiya inakwenda kuanguka ,kuna mchawi

    ReplyDelete