Promote your business for free

THIS BLOG IS SPONSORED BY AFRICAN SOCIAL NETWORK ,THE SOCIALY NETWORK PAY ITS USER IN POINTS BASED JOIN NOW AND SEE HOW MUCH MONEY YOU CAN MAKE USING SOCIAL NETWORK. | FEEL FREE TO ADVERTISE ON WWW.BONGLOB.COM

Wednesday, 21 July 2010

Ahsante Jumuiya ya Ki-Tanzania Reading (UK)



Wapendwa wana Reading,

Ninapenda kuchukua nafasi hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa ushirikiano wenu uliowezesha kufanikisha graduation yangu niliyohudhuria tarehe 02 July 2010 kwenye Chuo kikuu cha Reading (UK).

Kwanza ninaomba nijitambulishe, ninaitwa Mr. Bahati Mbwama Mbambe, mtanzania ninafanya kazi nchini Benin (Afrika Magharibi). Mwaka 2005, nilijiunga na Chuo Kikuu cha Reading na nimesoma course ya miaka minne ya BSc in Quantity Surveying by distance learning, nilimaliza course Novemba 2009.
Chuo Kikuu Cha Reading (UK) huwa kinandaa Graduation mara mbili kwa mwaka. Mwishoni wa mwaka na katikati ya mwaka. Nilishindwa kuhudhuria iliyofanyika Desemba 2009 kwa kuwa sikuwa tayari nikaamua kuhudhuria ya mwezi wa Sita mwaka huu.
Mtu anaweza kujiuliza kuwa niliijuaje jumuiya ya ki-tanzania ya Reading (UK)?
Wakati ninaendelea kujiandaa na safari yangu ya kuja huko Uingereza mwezi wa nne mwaka huu katika pita pita yangu kwenye blogu ya michuzi nikaona tangazo la uchaguzi wenu. Kwa bahati nzuri hata email yenu ilikuwepo pale. Basi nikawatumia email kuomba ushirikiano wenu pindi nitakapo kuja huko. Nilijibiwa baada ya muda mfupi kwa niaba ya jumuiya na Bwana Hussein Chang’a. Ambaye alinihakikishia ushirikiano wenu pindi nikiwa tayari kuja huko.
Muda ulipowadia nilimpigia simu bwana Hussen na alikuja kunipokea Heathrow Airport. Sikuamini macho yangu jinsi mambo yalivyokuwa yamerahisishwa kwa msaada wa jumuiya yenu ukizingatia ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kufika nchini Uingereza.
Tulipofika Reading, wakati tunaendelea kuzunguka kwenye maduka mbalimbali tulikutana na baadhi ya watanzania waishio Reading, wachache kuwataja ni Dr Cleopa, Mr Masuke, na wengine wengi ambao majina yao nimeyasahau utafikiri tulikuwa Dar Es Salaam (TZ). Kilichonifurahisha kila tuliekutana nae alionyesha moyo wa upendo wa ajabu ambao siwezi kusahau katika maisha yangu..
Baada ya muda mfupi tu nilikuwa mwenyeji Reading utafikiri nimekaa wiki nzima, nikatembelea Chuo pamoja na sehemu za biashara zinazoendeshwa na watanzania kama Vicent PUB ambapo nilikutana na Bwana Alan Kalinga na watanzania wengine.. Wote wanipokea kwa moyo wa ukarimu sana.

Graduation ilkuwa tarehe 02 July, 2010, na kwa mara nyingine tena wana Reading mlikuja kunipambamba utafikiri nilikuwa Tanzania.

Ninapenda kutoa pongezi zangu kwa Mwenyekiti wa jumuiya Bwana Davis Banduka na Katibu wake bwana Amri Dello, pamoja na viongozi wengine. Bila kuwasahau wana Reading kwa ujumla kwa utaratibu mzuri mliojiwekea wa kuindesha jumuiya yenu. Hata hivyo ni moyo wenu wa upendo mlionao ndio unawezesha mafanikio yenu.
Kama binadamu sina namna nzuri ya kuwashukuru wana Reading wote kwa mapokezi niliyoyapata kuanzia Airport na sehemu mbalimbali nilizopitia na kuonana nanyi. Nilipenda kuonana na Uongozi pamoja na wanajumuiya wengine wengi kwa sababu ya muda kuwa mfupi sikufanikiwa.
Kwa kuwa nimesoma hapo Reading ninaomba kama kuna shughuri zozote za jumuiya muwe mnanishikisha email yangu hii hapa chini.

Ahsanteni sana na Mungu awabariki sana katika shuguri zenu na karibuni Kotonu Benin (Afrika Magharibi)

Amen.

Bahati M Mbambe
SOGEA SATOM
MCA LOT 1 – Port of Cotonou Development Project
Cotonou
BENIN - WEST AFRICA
+229 95 33 75 04

















Picha ya pamoja na baadhi ya wana Reading baada ya graduation. Kutoka kushoto Hussein Changa , Rosemary,

Bahati Mbambe (mhusika) na Partrick Furlong (Rafiki yangu tulie soma wote chuo)





Picha ya pamoja na baadhi ya wana Reading baada ya graduation. Kutoka kushoto: Ni Ndugu Hussein Changa,, Gabinus Jumbe, Bahati Mbambe (Mhusika), Khalid Nsekela, Dada Rosemary na Ndugu Ali Magella

No comments:

Post a Comment