JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
UTANGULIZI
Kuna umuhimu mkubwa sana kwa kila Mtanzania kujua maana ya soko la
pamoja la Arrika Mashariki na taratibu zinazolizunguka soko hilo.
Kutokujua jambo hili ni hatua na dalili za awali za kushindwa
kukabiliana na changamoto zitazotokana na soko hili.Hii ni kweli
kwakuwa kama Mtanzania hajui nini maana ya soko la pamoja,ni maeneo
gani soko la pamoja au ushirikiano huu unahusika nayo na nini
kinafanyika na kwa vipi, bila shaka Mtanzania huyu hawezi pia
kushindana ma wenzake kutoka nchi washirika katika soko hili.
Kipeperushi hiki kimeandaliwa ili kumwezesha Mtanzania hasa Mtanzania
wa kawaida kuweza kujua hata kwa kiwango cha chini mambo ya msingi
yanayolizunguka soko hili ili iwe hatua ya awali kwake katika
kukabiliana na changamoto kutoka nchi washirika.
1. NINI MAANA YA SOKO LA PAMOJA LA AFRIKA MASHARIKI
Maana ya soko la pamoja la Afrika Mashariki , ni kiwango cha juu cha
ushirikano wa kiuchumi baina ya nchi washirika ambao unahusisha maeneo
nuhimu kama, uhuru wa kubadilishana bidhaa, uhuru wa kubadilishana
huduma,uhuru wa kubadilishana wafanyakazi, uhuru wa kubadilishana
mitaji na uhuru wa kuanzisha makazi popote katika nchi washirika.
Bidhaa ni kama mali zinazozalishwa viwandani mfano sabuni,dawa za
mswaki, matairi n.k., huduma ni kama tenda mbalimbali mfano tenda za
kutengeneza barabara, ugavi wa umeme,maji n.k. mitaji ni kama
uwekezaji katika sekta mbalimbali mfano kilimo,mabenki n.k. na pia
uanzishaji wa makazi na ukazi ni hatua ya mtu kutoka nchini mwake
kwenda kuishi kama raia mkazi katika nchi nyingine mshirika.
2. JE KUNA FAIDA GANI KWA TANZANIA KAMA NCHI KUINGIA KATIKA SOKO
HILI
Kwanza soko litaongeza ushindani katika biashara mfanO bidhaa za
viwandani jambo ambalo litawezesha kuzalishwa kwa bidhaa nyingi ,bora
na muhimu kwa watumiaji. Pia bidhaa hizo zitaweza kupatikana kwa
bei rahisi kutokana na ushindani mkubwa wa viwanda.
Pili soko litakuza ushirikiano imara ikiwa ni pamoja na kujenga
maelewano mema kati ya nchi washirika kupitia mwingiliano wa
wananchi na serikali zao na hivyo kuweka mazingira mazuri kisiasa na
kiuchumi katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Tatu soko hili litaweka uwanja mpana na mrefu utakaoinua wepesi wa
kuuza na kununua bidhaa.mazao na mali nyingine tunazohitaji, mfano
kama mkulima alikuwa anategemea kuuza mazao yake katika masoko ya
Tanzania tu na mikoa yake sasa mkulima huyu atakuwa na uwezo wa
kuogelea katika masoko yote ya Afrika Mashariki kwa kadri anavotaka na
anavyoweza.
Nne soko litatoa uwanja mrefu na mpana wa ajira.Hii ni kwasababu
Mtanzania aliyekuwa na uwezo wa kutafuta ajira Tanzania na mikoa yake
pekee sasa ataweza kutafuta ajira Rwanda ,Burundi na kwingineko kwa
uhuru.
Tano soko litakuza viwango vya utafiti katuka nyanja ya teknolojia na
maendeleo ya jamii. Hili linatokana na ukweli kuwa jamii ya Afrika
Mashariki itakuwa imeunganisha nguvu katika kutekeleza malengo haya
badala ya kila nchi kuhangaika na mambo yake kama ilivyokuwa awali.
Sita soko la pamoja litawaweka pamoja raia wa Afrika Mashariki na
hivyo kuondoa ubaguzi uliokuwa unasababishwa na mataifa haya
kutengana. Mganda atakuwa kama Mkenya na Mkenya kama Mtanzania
n.k.Hili ni muhimu kutokana na undugu wa kihistoria uliopo katuika
ukanda huu.
Kwa uchache sana hizi ndizo baadhi ya faida za soko hili.
3. SOKO HILI LINAHIUSISHA MAENEO GANI YA MSINGI
i. HAKI NA MWINGILIANO HURU WA WATU KATIKA NCHI WASHIRIKA
Ibara ya 7(1) ya mkataba wa makubaliano wa soko la pamoja inasema
kuwa wananchi wa nchi washirika watakuwa huru na haki ya kutembea
katika nchi wanachama. Kutokana na hili Mtanzania atakuwa huru na haki
ya kwenda Rwanda, Mkenya atakuwa huru na haki ya kwenda Burundi n.k.
• JE KUNA KIBALI CHOCHOTE AU KITAMBULISHO UNACHOHITAJI KUWA NACHO
KATIKA UHURU WA KUTEMBEA KATIKA NCHI WANACHAMA?
Ndiyo kutakuwa na hati maaalum(pass) atakayotakiwa kuwa nayo mtu
anapokuwa katika mwingiliano wa nchi wanachama. Hati hii ( pass)
inatolewa bure na itakuwa inadumu kwa miezi sita tu. Baada ya miezi
sita mhusika atatakiwa kuisajili upya(renew). Hii ni tofauti na
wananchi wengi wanavyodhani kuwa hakuna hati au nyaraka yoyote
inayohitajika unapotembea katika nchi washirika. Kwa wanafunzi hati
hii itakuwa inasajiliwa upya(renew) kila mwaka na sio miezi sita kama
ilivyo kwa raia wengine.
Pia katika mwingiliano huu kunaweza kukawa na mipaka au masharti iwapo
kutatokea hali tete ya usalama au hatari za kiafya kama magonjwa ya
kuambukizwa n.k. Katika hali kama hii uhuru wa kutembeleana unaweza
kuwekewa masharti.
UHURU WA KUFANYA KAZI POPOTE KATIKA NCHI WANACHAMA
Ibara ya 10(1) inasema kuwa wafanyakazi katika nchi washirika
watakuwa huru kufanya kazi popote ndani ya nchi washirika. Katika
kulitekeleza hilo tarehe 1. 7. 2010 kila nchi ilieleza ni wafanyakazi
wa aina gani imewafungulia milango, Mfano Burundi inahitaji wataalam
wa aina zote, Kenya mameneja,mafundi, na wataalam wengine, Tanzania
mafundi na wataalam wengine,Rwanda mafundi na wataalam wengine, Uganda
mameneja na wataalam wengine.
JE MFANYAKAZI ATARUHUSIWA KUFANYA KAZI HATA KATIKA OFISI ZA
UMMA(PUBLIC SERVICE) KATIKA NCHI WASHIRIKA?
Hapana mfanyakazi hataruhusiwa kufanya Kazi katika ofisi au huduma za
umma, kwa mfano hataweza kutoka mfanyakazi Uganda akajakuwa
mkurugenzi wa TAKUKURU au gavana wa benki kuu,mbunge,mkuu wa mKoa
n.k. Anaweza kupata nafasi hizo iwapo tu sera na sheria za nchi husika
zinaruhusu kitu kama hicho.
UHURU NA HAKI YA KUWEKA MAKAZI POPOTE KATIKA NCHI WASHIRIKA
Ibara ya 14(1) inasema kuwa raia yeyote wa nchi washirika ana haki ya
kuweka makazi popote katika nchi washirika. Mfano Mtanzania anaweza
kutoka hapa na kwenda kuishi Burundi, Mganda akaishi Kenya n.k.
JE UNA UHURU WA KUWEKA MAKAZI POPOTE KATIKA NCHI WASHIRIKA BILA KIBALI
AU KITAMBULISHO CHOCHOTE.?
Hapana kutatakiwa kibali maalum(residence permit) kitakachokuwa
kinatolewa kwa ajili ya ukazi katika nchi washirika.Sio kweli kama
wananchi walio wengi wanavyojua kuwa raia atakuwa anaweza kuishi
popote bila kibali au hati yoyote ya kumtambulisha.
JE RAIA ATAKAPOKUWA POPOTE NDANI YA NCHI WASHIRIKA ATALINDWA NA SHERIA
ZA NCHI YAKE AU SHERIA ZA NCHI ALIPOHAMIA NA KUWEKA MAKAZI
Ibara ya 14(7) inasema kuwa suala lolote linalohusiana ukazi wa raia
katika nchi washirika litalindwa na sera za nchi husika yaani nchi
alikohamia mtu na kuweka makazi ikiwa ni pamoja na sheria za nchi
washirika.Kwa hiyo raia atapaswa kufuata sera za nchi alikohamia
kwanza na kwa upande mwingine atafuata sheria za jumuia.
Ibara ya14(2) inatoa haki kwa raia aliyepata ruhusa ya ukazi katika
nchi washirika kutumia hiyo haki hata kwa familia yake. Ina maana
haki ya ukazi ya baba inatumika hata kwa mtoto pamoja na mke wake.
UHURU NA HAKI YA KUPATA NA KUTUMIA ARDHI KATIKA NCHI WASHIRIKA
Ibara ya 15(1) inatoa haki kwa raia wa nchi washirika kununua na
kutumia ardhi katika nchi washirika. Ina maana Mtanzania ataweza
kumiliki ardhi Uganda, Burundi n.k. Vivyo hivyo Mganda au Mnyarwnda na
wengine wana haki ya kuimiliki ardhi Tanzania n.k. .
UHURU NA HAKI YA KUBADILISHANA HUDUMA KATIKA NCHI WASHIRIKA
Ibara ya 16(1) inatoa haki na uhuru wa raia pamoja na setrikali za
nchi wanachama kubadilishana huduma. Ubadilishanaji wa huduma upo kama
ifuatavyo:
Kwanza ugavi wa huduma kutoka nchi moja mshirika kwenda nchi nyingine
mshirika, mfano Uganda inaweza kugawa umeme Tanzania au Tanzania
inaweza kutoa ugavi wa maji Rwanda na mazingira mengine kama hayo.
Pili ugavi wa huduma wa nchi mshirika kuwahudumia wageni au watumiaji
wa huduma wanaofika katika nchi ile, mfano Tanzania kutoa huduma ya
utalii kwa wageni kutoka nchi washirika au Uganda kutoa huduma ya
elimu kwa wageni au watumia huduma hiyo wanaofika eneo lile n.k.
Tatu ni aina ya hudum zitakazokuwa zinatolewa na mashirika pamoja na
taasisi maalum za kihiduma katika nchi washirika. Mashirika na taasisi
hizi wanaweza kutoa huduma zozote kulingana na sera na sheria za nchi
husika.
Nne ni huduma zitakazokuwa zinatolewa na watu binafsi yaani raia
wenyewe wa nchi hizi popote katika nchi wanachama,mfano mtu binafsi wa
Tanzania atakuwa na uwezo labda wa kutoa huduma ya usafi katika
barabara fulani ndani ya nchi washirika, makampuni ya mawakili watatoa
huduma zao katika nchi wanachama,madaktari ,wahasibu na mainjinia nao
wataweza kutoa huduma popote katika nchi washirika.
Ibara ya 17 imazuia aina yoyote ya ubaguzi katika tenda za utoaji
huduma kwa kueleza kuwa kila nchi itapaswa kuiangalia nchi nyingine
kama inavyojiangalia yenyewe.
Pia nchi washirika zimekubaliana kuendelea kufungua sekta
ndogondogo kutoka katika sekta za biashara na taaluma,
mawasiliano,ugavi,elimu na fedha, utalii na huduma za safari na
usafirishaji.
UHURU NA HAKI YA KUWEKEZA MITAJI KATIKA NCHI WASHIRIKA
Mfano wa maana ya kuwekeza mitaji ni kama raia wa Kenya kununua
mashamba Tanzania,Rwanda au pengine, au raia katika nchi washirika
kujenga kiwanda au benki n.k
Ibara ya 24(1) inatoa haki hii ikiwa ni pamoja na sharti la kuondoa
vikwazo katila uwekezaji wa mitaji.
JE KWA SASA RAIA WA NCHI WASHIRIKA WANAWEZA KUWEKEZA MITAJI TANZANIA?
Hapana jambo hilo kwa saa haliwezekani. Kwa sasa jambo hilo
linawezekana Rwanda, Uganda na Kenya. Tanzania pamoja na Burundi
wameahidi kuruhusu uwekezaji wa mitaji katika kipindi hiki cha 2010
mpaka 2015.
JE USALAMA WA WATUMIA BIDHAA(RAIA) UMEZINGATIWA KUTOKANA NA USHINDANI
WA UZALISHAJI UTAKAOKUWEPO
Kwakuwa utakuwepo ushindani mkubwa katika uzalishaji hasa sekta ya
viwanda jumuia imeona ni muhimu kuweka uataratibu maaluma wa kulinda
usalama wa raia mtumia bidhaa. Ibara ya 36(1) inasema kuwa nchi
washirika zinapaswa kutanguliza mbele maslahi ya watumiaji wa bidhaa
ili kuwahakikishia afya na maisha bora na pia kuhakikisha ushindani wa
kibiashara inakuwa nyenzo ya raia kupata bidhaa kwa bei nafuu.
MATENDO YA KIBIASHARA YALIYOPIGWA MARUFUKU KATIKA SOKO LA PAMOJA
Ibara 33(1) inapiga marufuku tendo lolote linalolenga kuathiri uhuru
wa kibiashara
Ibaa ya 34(1) inapiga marufuku tendo lolote lialolenga kuzuia au
kuharibu ari ya ushindani katika soko.
Ibara vya 35 inazuia tendo lolote la ubaguzi katika ugavi wa huduma
pamoja na bidhaa katika nchi washirika
SEKTa NYINGINE MUHIMU ZILIZOLENGWA NA SOKO HILI
Kilimo na chakula, ushirika na maendeleo ya viwanda,uchumi na
muunagano katika sera za kifedha,usafirishaji na huduma nyingine za
kijamii,utafiti na maendeleo ya teknolojia, kulinda hakimiliki na na
ushirikiano wa kitakwimu na sekta nyinginezo.
No comments:
Post a Comment